Image
Image

Serikali yafuta hati 5 za umiliki wa ardhi zilikuwa zinamilikiwa na raia wa Uingereza.


Dar es Salaam. Serikali imefuta hati 5 za umiliki wa ardhi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na raia wa Uingereza aliyetajwa kwa jina la Hamant Patel mkazi wa Mwanza baada ya kugundulika kughushi cheti cha kuzaliwa na kujitambulisha kama raia wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuki amesema hati hizo zilizofutwa zilitolewa kwa udanganyifu kwa mmiliki huyo katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu.
Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria za nchi raia wa nje hawaruhusiwi kumiliki ardhi na kwamba wanayo fursa ya kupata ardhi kupitia kituo cha uwekezaji nchini (TIC).
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment