Image
Image

Majaliwa atoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kumpa maelezo sababu za Tanzania kutokukamilisha Mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao.
Alitoa agizo hilo wakati akimwakilisha Rais John Magufuli katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
"Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo.
"Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na si Mwanasheria wa Tanganyika Law Society peke yake, kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu," alisisitiza.
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyopewa kuhusu mkataba huo, utakuwa na umuhimu mkubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kama ilivyo kwenye sekta nyingine zinazoshirikiana ikiwemo uhandisi, uhasibu, uthamini na uchoraji wa majengo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wanasheria hao kuzisaidia nchi zao ili ziondokane na umasikini uliokithiri na Serikali zipate muda wa kushirikisha watu wake katika kufanya kazi kwa lengo la kuwapatia maendeleo. Alisema nchi zilizoendelea na zinazoendelea, baada ya chaguzi hufanya shughuli za ujenzi wa taifa lao na maendeleo ya watu wake. Ili kudumisha demokrasia wana muda wa mikutano na maandamano na kazi.
“Mfano kifungu cha 115 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kinataka kesi zinazotokana na uchaguzi ziwe zimefunguliwa mahakamani ndani ya siku thelathini tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na ziwe zimesikilizwa na kutolewa maamuzi ndani ya miezi kumi na miwili tangu tarehe ya kufunguliwa mahakamani," alisema.
Aliongeza kuwa; "kwa uelewa wa kawaida, kifungu hiki ni kuwa jamii inataka masuala ya siasa za uchaguzi yawe na muda wake wenye ukomo maalumu ili baada ya hapo wananchi waelekeze muda, nguvu na rasilimali zao nyingine katika kazi au shughuli nyingine za maendeleo na ujenzi wa Taifa lao."
Alisema eneo jingine ambalo ni muhimu kulitupia jicho ili kukuza ushindani wa kibiashara katika Jumuia ya Afrika Mashariki ni la uendeshaji wa mashauri mahakamani hasa kwa mashauri ya madai.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment