Spika
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Tano wa Bunge la
11 utakaoanza kesho mjini Dodoma.
Na
Jacquiline Mrisho na Eleuteri Mangi – MAELEZO, DodomaMkutano
wa Tano wa Bunge la 11 wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania
unatarajiwa kuanza kesho Novemba 01 hadi Novemba 11 mwaka huu.
Taarifa
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Spika wa Bunge, Job Ndugai alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya shughuli mbalimbali
zitakazofanywa na bunge kutokana na ratiba itakayotolewa kulingana na
Kanuni ya 64.
“Hali
ya Bunge ni shwari na salama, nawasihi wabunge ambao bado hawajawasili
Dodoma waje ili tuweze kuifanya kazi ya kuishauri Serikali”, amesema
Mhe. Ndugai.
Spika
ameyataja baadhi ya majukumu yatakayotekelezwa katika Mkutano wa Tano
wa Bunge la 11 kuwa ni pamoja na kujadili, kupokea na kutoa maoni
kuhusiana na muongozo wa kuandaa Bajeti ijayo ambapo katika mjadala huo
Serikali itapata ushauri kuhusu vyanzo mbalimbali vya mapato na kupata
ushauri kutoka kwa wabunge kuhusiana na vipaumbele ambavyo vitatiliwa
mkazo katika uandaaji wa Bajeti ya mwaka 2016/2017.
Kazi
zingine zitakazofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kipindi cha
maswali yatakayoelekezwa kwa Serikali na kupatiwa majibu kutoka wizara
mbalimbali na taasisi zake, isipokuwa siku ya Alhamisi ambapo maswali ya
papo kwa papo yasiyozidi 10 yataelekezwa kwa Mhe. Waziri Mkuu ambayo
atayapatia majibu.
Aidha,
Spika amesema kuwa katika mkutano huo, Bunge litapokea taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na majibu ya
Serikali kuhusiana na taarifa hiyo pamoja na taarifa za kamati mbili za
fedha ambazo ni Kamati ya Fedha za Serikali na Kamati ya Fedha ya
Serikali za Mitaa kuhusu kazi walizofanya kulingana na hesabu
zilizokaguliwa na CAG kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kwa lengo la kujadili
matumizi ya Serikali baada ya matumizi hayo kufanyika.
Vile
vile katika mkutano huo Bunge linatarajia kupata siku moja ili wabunge
wajadili mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Ulaya (EU) ambao ni
muhimu kwa maslahi ya nchi ikitarajiwa wabunge wataishauri Serikali
endapo Tanzania iridhie kuingia mkataba huo au isiridhie kulingana na
ushauri utakaolewa na wabunge ambapo Serikali itakuwa ndiyo muamuzi wa
mwisho wa suala hilo.
Ameongeza
kuwa Bunge hilo litapokea Miswada miwili itakayowasilishwa ukiwemo
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria
ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 3 wa mwaka 2016.
Kuanza
kwa mkutano huo kunafuatia kumalizika kwa vikao vya Kamati za Kudumu za
Bunge vilivyofanyika kwa muda wa wiki mbili mjini Dodoma ambapo kamati
hizo zilikutana na kujadili mambo mbalimbali ya kuishauri Serikali
katika azma ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment