Dar es Salaam. Wahariri
wa vyombo vya habari nchini wamemuomba Rais John Magufuli aingilie
kati na kuagiza Muswada wa Sheria ya Huduma kwa vyombo vya Habari
usiwasilishwe katika Bunge litakaloanza leo hadi wadau wapate fursa ya
kuujadili.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba kudhamiria kuharakisha kupeleka
muswada huo bila kushirikisha wadau.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
limependekeza muswada huo upelekwe katika Bunge la Februari 2017 badala
ya wiki hii kwa kuwa una kasoro nyingi ambazo zinatakiwa kujadiliwa kwa
kina na endapo kamati ya Serukamba itaupeleka bungeni basi hautakuwa
umeshirikisha wadau.
Katika
mjadala wao jana, wahariri hao walisisitiza kuwa suala la kuwafikia
wadau wote wa muswada huo linahitaji muda zaidi, huku mjumbe wa bodi ya
TEF, Jesse Kwayu akieleza wasiwasi wake jinsi Serukamba anavyolisukuma
suala hilo.
0 comments:
Post a Comment