Image
Image

Wakurugunzi wa 5 wenye kiwango cha chini cha elimu na mameneja kung'olewa ATCL

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imeeleza kuongezeka kwa makusanyo ya shirika hilo katika kipindi kifupi cha uendeshaji wake kutokana na kudhibitiwa kwa mapato na matumizi.
Aidha bodi hiyo imeagiza kuwaondoa wakurugenzi watano na baadhi ya mameneja katika nafasi zao kwa kuwa wengi wao wana viwango vya chini vya elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao hivyo kusababisha utendaji wa kazi kuwa dhaifu.
Kutokana na hatua hiyo, bodi hiyo imemuagiza Ofisa Mtendaji Mkuu kutangaza nafasi zote za wakurugenzi na mameneja zilizo wazi na zile zenye wafanyakazi wenye utendaji dhaifu kwa kuzingatia muundo wa muda uliopitishwa na bodi hiyo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo ya ATCL, Emmanuel Korosso alipokuwa anazungumzia masuala yanayoihusu kampuni hiyo.
Akizungumzia kuimarika kwa makusanyo, Korosso alisema; Katika kipindi kifupi tangu kuanza kwa safari za ndege mpya tumeweza kudhibiti mapato na matumizi na kumekuwa na ongezeko la mapato ya uzito wa ziada wa mizigo.
Kuhusu kuondolewa kwa wakurugenzi na mameneja, Mwenyekiti huyo wa bodi alisema bodi hiyo imeagiza kuwa wakurugenzi na mameneja waliokuwa wamethibitishwa kazini lakini hawana sifa kuondolewa katika nafasi zao na kupangiwa majukumu mengine kulingana na sifa zao.
Mwenyekiti huyo wa bodi alisema muundo wa muda unataka uwepo wa wakurugenzi watatu tu katika uendeshaji wa kampuni hiyo.
Akizungumzia baadhi ya maboresho, Korroso alisema katika matumizi ya tiketi za bure au zilizopunguzwa bei, bodi imeagiza Menejimenti ya ATCL kusimamisha kwa muda Mkataba wa Hiari baina ya Menejimenti na wafanyakazi na sasa watapewa tiketi za bure na tiketi yenye punguzo mara moja kwa mwaka kama stahili ya likizo.
Kuhusu idadi ya wafanyakazi Korosso alisema hivi sasa shirika hilo linao wafanyakazi 221 na wanalenga wakiwa na ndege zao zote watakuwa na wafanyakazi 350.
Alisema baada ya kupokea ndege mpya mbili aina ya Bombardier Q400 na kuanza safari Oktoba 14 mwaka huu katika kumekuwepo na changamoto ya ucheleweshaji wa ndege na pia kutokutoa huduma kwa maeneo yaliyopaswa kufikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment