Image
Image

TANZIA:Mpiga picha wa NIPASHE na The Guardian afariki jijini Dar es Salaam.

Mpiga Picha Mwandamizi wa magazeti ya Nipashe na The Guardian, Mpoki Bukuku(Pichani) amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari akivuka barabara Mwenge jijini Dar es Salaam.
Habari zinaeleza kuwa mara baada ya kugongwa na gari alipata wasamaria wema ambao walifanikiwa kukodi bajaji kumpeleka hospitali kusudi aweze kupatiwa huduma ya kwanza, ambapo walifika hospitali ya Mwananyamala na maelezo yanadai waliambiwa wampeleke muhumbili kwani huko ndio sehemu husika nayenye kumpatiba mujarabu kwa namna alivyogongwa na gari na kuumia.
Marehemu Bukuku ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake ambapo inaelezwa kuwa alivunjika miguu yote miwili na mkono na kisha kukimbizwa  Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha mifupa MOI kwa ajili ya matibabu. 
Hata hivyo taarifa zilizotufikia zimedai kuwa Marehemu Mpoki Bukuku aligongwa na gari ambayo haikuweza kufahamika mpaka sasa usiku wa 22 Desemba 2016 wakati anatoka ofisini kuelekea nyumbani kwake.
Uongozi wa Tambarare Halisi unatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na Tasnia nzima ya Habari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment