Image
Image

Wafugaji 25 waliokaidi agizo la Mkuu wa Mkoa mkoani Rukwa waondolewa kwa nguvu.

SERIKALI ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imewakamata na kuwarudisha kwa nguvu wafugaji 25 walikotoka wakiwa na ng’ombe 2,000, wakidaiwa kukaidi amri halali ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven kwa kuingia kinyume cha utaratibu wilayani humo.
Aidha, Mwenyekiti na Mtendaji wa Kijiji cha Kisaila kilichopo katika Kata ya Samazi mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani humo, wamekamatwa na kushikiliwa kwa saa kadhaa kwa kukiuka agizo hilo la mkuu wa mkoa, ambapo waliwaruhusu wafugaji kuingia mifugo yao kinyume cha utaratibu kijijini humo.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura alipohutubia mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Mwimbi na Mwambekenya, ambavyo vimekumbwa na migogoro ya ardhi iliyosababisha mauaji ya wafugaji wawili.
Binyura alisema wafugaji na mifugo hiyo iliingia kinyemela wilayani humo ikitokea katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga hivi karibuni.
Alipiga marufuku kwa wakazi wa wilaya hiyo kuuza ardhi holela kwa wafugaji bila kufuata utaratibu, akisisitiza kuwa wilaya hiyo haiko tayari kupokea tena mifugo inayotoka nje ya wilaya hiyo.
Alisema tamaa ya fedha kwa wakulima kuwauzia maeneo ya ardhi wafugaji kwa ajili ya malisho ya mifugo yao, kumesababisha si tu migogoro ya ardhi, bali pia ubaguzi na ukabila baina ya jamii hizo mbili.
Alisisitiza kuwa taratibu za kuwaruhusu wafugaji kuingiza mifugo wilayani humo hazikufuatwa, ambapo sasa wakulima wanataka kuwafukuza wafugaji kwenye maeneo ambayo waliwauzia alisisitiza kuwa hiyo haiwezekani.
Kwa upande wa wakulima, aliwaonya waache tabia za kuswaga mifugo ya wafugaji kwenye mashamba yao ili walipwe fidia ambayo huwa kati ya Sh 200,000 hadi Sh 600,000 kulingana na ukubwa wa eneo. Naye Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisisitiza kuwa wilaya hiyo haina eneo la ziada la ardhi kwa malisho ya mifugo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment