Image
Image

MAJALIWA:Uongozi wa wizara ya Elimu, TAMISEMI chunguzeni kufeli wanafunzi Mtwara.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wizara wa Elimu Sayansi na  Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu  zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili 
kutoka mkoani humo.
Piaameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili  kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha 
ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.
WaziriMkuu ametoa agizo hilo Januari 17, 2017 wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya  Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Kwamujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya
kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. 
Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa,  Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya 
Tanga ikiwa ni Nywelo.
“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara,wakafuatilie kwakina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.
Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri  Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo  mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo 
hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.
Awali,akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali 
Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha 
pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa 
na mkoa wa Geita.
Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja  kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment