Image
Image

Rais Mteule wa Marekani Donald Tump kuapishwa leo kuwa rais wa 45 wa Taifa hilo.

Rais mteule wa Marekani aliyechaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba 2016 Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017.
Bw Trump wa chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.
Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.
Ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.
Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.
19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.
20:00 Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.
Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.
Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment