Image
Image

Serikali kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana stadi za kazi.

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Ally Msaki (kulia), makubaliano hayo ni kati ya Taasisi hiyo na Serikali ili kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya ngozi.
Na Fatma Salum-MAELEZO
Serikali imepanga kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana stadi za kazi 
zitakazowawezesha kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa 
Viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini 
makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam 
(DIT) na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na 
Wenye Ulemavu.
Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki amesema kuwa 
yatasaidia kuiwezesha Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa vijana hasa ya 
kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi ili waweze kushiriki katika ujenzi 
wa uchumi wa viwanda.
“Vijana 1000 wataanza kupata mafunzo mwezi Februari mwaka huu na yatakayohusu utengenezaji wa bidhaa za ngozi na program hii ipo ndani ya mpango wa miaka mitano.” Alisema Msaki.
Mafunzo hayo ya stadi za kazi kwa vijana yatagharimiwa na Serikali na 
yatahusisha vijana walio katika mfumo rasmi na wale wasio katika mfumo 
rasmi wa elimu lengo likiwa ni kuwakwamua vijana ili washiriki 
kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment