Image
Image

Serikali yatoa sh. bilioni 2.4 kuboresha mradi wa maji Makambako mkoani Njombe.

Picha kwa hisani ya Maktaba.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 2.4 kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji katika mji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Polisi Makambako mkoani Njombe Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi za salama katika umbali usiozidi mita 400 kama inavyosema sera ya maji.
Aidha  amewataka wananchi kutofanya shughuli za kijamii katika vyanzo vya maji ili kuvilinda na kusisitiza  Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta maji kwa sababu vyanzo vingi zimekauka kutokana na shughuli za kibinadamu.
Awali  akizungumzia madai ya Fidia kwa wananchi  waliopisha ujenzi wa kituo cha ukaguzi cha pamoja na soko la kitamaifa katika eneo la Makambako  amesema sewrikali itawalipa fidia.
Nae Mbunge wa jimbo la Njombe Mheshimiwa SANGA amesema moja ya changamoto inayowakabili wakazi wa mji wa Makambako ni ucheleweshwaji wa malipo ya fidia kwa waliopisha ujenzi wa kituo hicho hali inayosababisha baadhi yao kwenda kudai fidia hiyo kwa kiongozi huyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment