Image
Image

Timu ya Manchester United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita.

Timu ya Manchester United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita kulingana na taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani (Deloitte).
Manchester United imewashinda Real Madrid waliofanya vizuri katika michezo kwa miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa takribani Euro 689 katika msimu wa 2015-2016.
Clubu za ligi ya Premier imeshuhudia kukua kwa kipato kwa Euro Millioni mia moja.
Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.
Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano kwa kutengeneza Euro milioni524 kwa msimu uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa city kuingia katika nafasi hiyo.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment