Image
Image

Waziri mkuu aahirisha ziara yake mkoani njombe mpaka January 25.

Waziri mkuu Majaliwa akizungumza na wakazi wa njombe Maeneo ya Hospitali ya Mkoa wa njombe Mtaa wa Wikichi Njombe Mjini.
Baadhi ya wakazi wa Njombe Mjini wamiwa wanamsikiliza waziri Mkuu Kassm Majaliwa katika maeneo ya Wikichi Mjini Njombe
Wziriri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha chai cha Kibena 
Na Mwandishi wetu
WAZIRI  Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ameahirisha ziara yake mkoani Njombe nakurudi jijini Dar es salaam kumpokea Rais wa Uturuki Recep Erdogan ambaye amekuja kwa ziara ya kikazi ya Siku Mbili ambapo Ziara ya waziri mkuu majaliwa inatarajiwa kuendelea januari 25 kwa siku tatu.
Waziri mkuu amekuwa mkoani Njombe kwa siku tatu ambapo amepita katika halmashauri tatu za mkoa huo kabla ya kuahirisha ziara hiyo na kurejea jijini Dar es Salaam kwa majukumu mengine ya kiutendaji ziara yake mkoani Njombe ilikuwa ya siku sita na kuzitembelea halmashauri zote za mkoa huo.
Waziri mkuu Juzi aliwaaga viongozi wa mkoa wa Njombe na kuelekea jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya ndege mkoani Iringa huku akitarajia kulejea tena mkoani humo Januari 25 na kumaliza ziara yake baada ya siku tatu.
Akirejea Njombe atatembelea halmashauri ya wilaya ya Njombe na kutembelea kiwanda cha chai na kuzungumza na wakulimqa wa zao hilo, kasha kuzungumza na wakazi wa Mji wa Njombe baadaye kwenda wilayani Ludewa ambako pia atakutaa na wakazi wa Mundini na Liganga kutako tarajiwa kuwa na migodo ya makaa yam awe na Chuma.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akizungumza na Nipashe kuhusiana na kuahirishwa kwa ziara hiyo alisema kuwa waziri mkuu alikuwa mkoani humo kwa siku tatu ambapo ameahilisha kuendelea na ziara na kasha kulejea tena Januari 25.
Alisema kuwa waziri mkuu anaelekea jijini Dar es Salaam kwa kuwa nchi itakuwa ikipokea ugeni wa Rais wa Uturuki ambaye anafanya ziara yake hapa nchini ambapo baada ya ziara ya Rais Huyo Waziri mkuu watalejea Mkoani Njombe.
Mwishoni mwa wiki jana Waziri mkuu alikuwa mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa maeneo mbalimbali ya halmashauri za wilaya Makete, Wangingombe, na mji wa Makambako ambako ndio alianzia ziara yake.
Akiwa Wangingombe alifungua jingo la Halimashauri ya Wangingombe na kuzungumza na wananchi wa Mjia huo kasha kuwataka watumishi wa halmashauri na wilaya kuhamia halmashauri hiyo ifikapo mwezi februari.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment