Image
Image

Lates News:Wema Sepetu na mama yake wang'atuka CCM na kuhamia CHADEMA.

Wema Sepetu ambaye alikuwa ni kada wa CCM kwa muda mrefu atangaza rasmi kukihama chama cha CCM na kuhamia CHADEMA, huku akiweka wazi kuwa ameamua kwa dhati ya moyo wake bila kushawishiwa na mtu yeyote ni maamuzi.
Amesema baada ya tuhuma za kuhusishwa na Sakata la dawa za kulevya ambazo hazikuwa na ukweli wa kina ni tuhuma zimemnyong'onyesha mnoo,amaesema kuhamia chadema hajapewa hata shilingi kumi.
Muda huu wema anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo licha ya uamuzi huo wa wema pia mama yake mzazi naye ameng'atuka na kujiunga CHADEMA ambapo wamerudisha kadi rasimi za CCM.
Wema: Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham.
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe
Wema: Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nataka kuhamia Chadema kutoka CCM.
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Nyote mnajua nlikuwa kada wa ccm na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote.
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazimutosha na sikufa moyo.
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM.
Wema: Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na nliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana
Wema: ⁠⁠⁠Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu
Wema: ⁠⁠⁠Nimetafakari sana kwanini hili limetokea
Wema: ⁠⁠⁠Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani
Wema: Mimi naamin katika demokrasia. Nmefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu
Wema: ⁠⁠⁠CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
Wema: ⁠⁠⁠Ningejua mapema ningeniunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA
Wema: Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono.
Wema: ⁠⁠⁠Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu
Wema: ⁠⁠⁠Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini
Wema: ⁠⁠⁠Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.
Tangu leo mimi sio mwanachama wa CCM. Mimi na mama tulikuwa wanachama hai wa CCM.
Kwa upande wake mama Sepetu, alikuwa na haya ya kusema;
Mama Sepetu :Mmekuwa mnasema natoa mapovu,mimi sitoi mapovu
Mama Sepetu :Uchungu wa mwana aunuae mzazi
Mama Sepetu :Nmehangaika sana mwanangu alipowekw ndani
Mama Sepetu :Ningejua mapema ningeniunga chadema zamani. Mama Sepetu :Najilaumu sana ku helewa jiunga chadema.
Mama Sepetu :Hakuzungumza yeye mimi sasa ndo nguli nazungumza
Mama Sepetu :Ametuhumiwa sana. Amekaa sero hamjamuona mwanangu akiwa alosto
Mama Sepetu :Hamna kiongozi wa ccm alokuja kuniuliza kulikoni
Mama Sepetu :Mpaka usiku walikuwa wanafuatwa mahabusu na makonda
Mama Sepetu :Haki za binadamu hazimuzingatia, watu wanaua wanapewa dhamana
Mama Sepetu :Lakini yeye kahangaishwa chana
Mama Sepetu :Mimi ni mkt wa ccm tawi la nzasa kata k/nyama tulikuwa na kura nyingi 2015
Mama Sepetu :Wengi hataki kuzungumza wanauguliwa sana
Mama Sepetu :Sisi ni watanzania tumepanwa tupo kwenye kitanzi
Mama Sepetu: Mimi kama mama nmesema siwezi kuteswa na mwanangu kudhalilishwa tukiwa chama cha mapinduzi
Mama Sepetu: Mwanangu amezunguka na ccm anainadi nchi nzima
Mama Sepetu :Tangu leo mimi sio ccm tena. Na ntatembea nchi nzima kukinadi chama cha demokrasia na maendeleo
Mama Sepetu :Nashangaa chadema hawatupi kadi zao.
Mimi ni mwenyeji wa Singida. Baba katuacha tupo 72. Naenda kupokea kadi za CCM Singida na wote wameahidi kuhamia chadema
Wema: Naomba maswali matatu yanayohusiana na mimi kuhama
Swali: Unaidai CCM?
Majibu ya Wema: Wasanii wengi ikiwemo mimi nawadai, nikianza kuzungumzia madeni watasema ni kwa sababu tumehama. Mimi na wasanii wengine tunawadai CCM lakini wanatujibu tukamdai Kikwete rais mstaafu.
Mariam anauliza swali kuhusu voice note
Majibu: Mimi siku nyingi nimezima simu yangu, sijui wala sijaangalia kitu gani kimezungumzwa. Japo kuwa nmesikia kwamba kuna sauti. Siijui kabisa
Mimi simu yangu ina matatizo, siwezi kuisikiliza hiyo sauti, mlioisikia ni nyinyi sio mimi
Steve ni mtoto wangu sasa hiyo sauti yangu na Steve siijui
Wala sijawahi kuisikia ila nina mpango wa kuisikiliza simu ikipona
Je huu uamuzi ni wa hasira?
Wema: Hapana sio wa hasira, nimepata hasira kura za viti maalum na ndo ningehama. Hadi hapo CCM ilipo ina jasho langu na nguvu zangu. 
Nimeonewa na imefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama
Nilijitoa ikibidi nife. Nilipoenda Zanzibar wanachama wa CUF walitaka kunimwagia tindikali kisa mimi ni wa CCM. Walinimwagia michanga. Hiyo yote ni katika harakati za kuitetea CCM
Leo chama ndo kimefanya nipitie yote Haya
Mapenzi ni nipe nikupe, mapenzi yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi
Je chadema wamekununua? 
Majibu: Chadema hawajanipa hata sh 10. Ni mapenzi yangu tu. Hayo mambo ya fedha tumezoweshwa kwa sababu chama cha mapinduzi ndo mtindo wao.
Huu ni uamzi mgumu sana, na mimi nikishasema basi ni basi. Sirudi nyuma.
Chadema wanapigania demokrasia. Tanzania yetu imeanza kupoteza demokrasia kwa kiasi kikubwa.
Sijaingia kwenye mitandao. Natamani niingie na kutoa kale kapicha ka CCM nilichokipost tatizo sijapata muda wa kuingi kwenye mitandao. 
Kama ni vita nimeshavaa magwanda nipo tayari kupigana 
Chadema wamenipokea kwa mikono miwili 
Swali: Kuna mtu mkubwa una bifu naye, CCM unafanyiwa hivi, je chadema si itazidi?
Kwanza kabisa sina bifu na mtu yoyote kutoka CCM 
Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge 
Kumbuka mimi nina kesi mahakamani, tunachopigania ni uhuru na demokrasia. ..........................
Zaidi tizama hapa kuona tukio zima.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment