Image
Image

Polisi yathibitisha kumshikilia Masogange kwa tuhuma za uuzaji ama utumiaji dawa za kulevya.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia video queen' Agnes Gerald maarufu kwa jina la 'Masogange', kwa kuuza ama kutumia dawa za kulevya na hivyo idadi ya watuhumiwa mpaka sasa kufikia 349.
                           Agnes Gerald maarufu kwa jina la 'Masogange'
Amesema licha ya watuhumiwa pia jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na watakuwa mbaroni wakati wowote.
Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani leo.
Hata hivyo Sirro ametolea ufafanuzi Kuhusu askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, amesema askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Sirro ameongeza kuwa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na kuwatuhumu kuwa wanahusika na uuzaji ama utumiaji wa dawa za kulevya.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment