Image
Image

Tanzia:Mchezaji wa Yanga Godfrey Bonny afariki .

Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny amefariki , baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Bonny maarufu kama Ndanje, amefariki dunia baada ya kulazwa muda mrefu katika Hospitali ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya.
Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo.
“Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki. Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga,” alisema.
Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Prisons.
Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambako alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment