Image
Image

Trump azungumza kwa njia ya simu na rais wa china kuheshimu sera ya china moja.

Rais Donald Trump wa Marekani anairidhisha China katika suala la Taiwan. 
Akizungumza kwa simu na rais wa Jamhuri ya umma wa China, Xi Jinping, rais Trump anasemekana amehakikisha ataheshimu sera ya China moja. 
Serikali ya mjini Beijing inaiangalia Taiwan kuwa ni sehemu ya ardhi yake. 
Duru za ikulu ya Marekani zinasema viongozi hao wawili wamealikana kila mmoja kuitembelea nchi ya mwenzake. Mazungumzo hayo yalikuwa ya kwanza kufanyika kati ya viongozi hao wawili tangu Donald Trump alipoapishwa kuwa rais wa Marekani, Januari 20 mwaka huu. 
Baada ya kushinda uchaguzi wa rais Trump aliwakasirisha viongozi wa China, aliposema amepokea risala ya pongezi kutoka kwa rais wa Taiwan na kuongeza kusema kwamba suala la Taiwan linaweza kufumbuliwa. 
Matamshi hayo yaliikera China na yalionyesha kwenda kinyume na mwongozo uliokuwa ukifuatwa kwa miongo kadhaa na serikali mjini Washington.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment