Image
Image

Uturuki ni mfano mzuri katika utatuzi wa masuala ya kimataifa.

Mojawapo ya masuala ambayo yalisubiriwa kabla ya Donald Trump kuingia madarakani ni mtazamo wake na hatua atakazozichukua kuhusiana na masuala ya Mashariki ya Kati.
Hata hivyo baada ya kukabidhiwa mamlaka Trump hakuchelewa kubainisha hatua atakazochukua kuhusu mizozo na masuala ya kanda ya Mashariki ya Kati.
Hatua alizochukua na mipango aliyoweka zimeonyesha msimamo mkali hata baada ya kuwa na haki ya mtafaruku duniani hapo awali iwapo Trump angekuwa rais wa Marekani. 
Kwa kawaida Marekani inajulikana kuwa nchi yenye nguvu zaidi duniani na kuonekana nchi ambayo mara nyingi huwa na serikali ya kuchukua hatua za kimabavu.
Lakini mwanzo kabisa baada ya Trump kuapishwa na kuingia ikulu, alifanya mazungumzo na mfalme wa Saudi Arabia na baada ya muda kidogo akaendelea na kumkaribisha mfalme Abdullah wa Jordan, isitoshe ni ziara ya kwanza kabisa ya mkuu wa idara ya upelelezi ya Marekani ya CIA Mike Pompeo.
Baada ya kuteuliwa kuwa mkui wa CIA Mike Pompeo alitekeleza ziara yake ya kwanza ya kimataifa katika nchi ya Uturuki mnamo Februari 8. 
Baadae Pompeo alielekea katika nchi ya Saudi Arabia na Bahrain.
Kando na hilo ni msisitizo wa rais Trump kuhusu kuwepo kwa kanda salama Syria na pia kuungana katika mapambano dhidi ya Daesh .Ishara ya kuwa serikali mpya ina azimio la kuwa na mpango mpya n wenye nguvu kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati. 
Kulingana na historia ya Marekani kuhusu sera yake kwa Mashariki ya kati imeonyesha kuleta madhara katika kanda hiyo. 
John Foster Dulles, waziri wa mambo ya nje zamani Marekani mwaka 1953 aliwahi kuzuru Mashariki ya Kati na baada ya ziara yake kanda hiyo ilikumbwa na vita kwa ajili ya sera mpya alizozindua kipindi hicho, mwaka 1956 Eisenhower Doctrine akaondoa sera hizo vita vikapungua lakini tena hali kama ya awali ikatokea tena miaka ya 1970 kipindi cha 
Henry Kissenger na baadaye pia kipindi cha Bush.
Hata hivyo utawala wa Serikali katika miaka ya nyuma uongozi nchini Marekani umeonyesha sera mbaya hasa katika masuala ya siasa za kimataifa.
Serikali ya Obama ni mojawapo za utawala wa awali wa Marekani ambazo zilidhihirisha kutofaulu katika kupata suluhu za mizozo inayokumba kanda ya Mashariki mwa Kati.
Hii ni sababu kuu ambayo katika uchaguzi mkuu chama cha Democrats kilishindwa na wafuasi wa chama cha Republicans kuongoza.
Sera za Obama zilizopelekea kuongezeka kwa migogoro katika kanda ya Mashariki ya Kati zilianzishwa mwaka 2010 na hii ndio sababu ya mwanzo wa vita vya ndani nchini Syria.Ili kutuliza hali hii Iran na Urusi ikaingilia kati na kufanya juhudi za kupooza hali hiyo.
Huku Marekani nayo ikiondoka Iraq, Iran nayo ilikuwa yajitahidi kuendelea kuathiri sera zake katika mataifa ya kiarabu na pia kuadhibu baadhi ya tawala zake.
Mnamo mwa 2015, Saudi Arabia ikaunda muungano wa jeshi la Kiislamu na kupelekea usitishaji vita nchini Yemen.
Serikali ya Marekani ya Obama kipindi hicho ikaanzisha sera ya 'kutazama na kuona' na huku maelfu ya raia wakiuawa Syria, vita nchini humo viliendelea kwa miaka 6 bila ya Marekani kuchukua hatua yoyote.Huku hali ikiendelea kuzorota, Urusi na Iran ikachukua uamuzi wa kujiondoa.
Serikali ya Marekani nayo kipindi hicho ikaunda kundi la PYD/YPG na kutoa msaada wa silaha kwake jambo ambalo lilizidi kuchafua hali nchini Syria.
Isitoshe baada ya kufanya hivyo wakaendelea kuvunja uhusiano wake na nchi ya Uturuki.Ni wazi kuwa Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikichukua hatua kimakosa hivyo basi sharti rais mpya wa Marekani Donald Trump kurekebisha baadhi ya makosa haya.
Serikali ya Obama mara nyingi imetumia sera ambazo ziliendelea kuharibu amani ya dunia hivyo basi ni sharti wapewe mafunzo na kuonyeshwa mfano.
Hii ndio kwa sababu Mike Pompeo alizuru Uturuki katika ziara yake ya kwanza kimataifa ili kuharakisha katika kufanikisha utumiaji wa sera mpya za Trump kwa masuala ya siasa za Mashariki ya Kati.Uturuki ni nchi ambayo imekuwa mfano mzuri kwa hatua zake za kuendeleza amani na utulivu katika maeneo tofauti ya Mashariki ya Kati hasa Syria baada ya kuanzisha operesheni ya Fırat dhidi ya magaidi kaskazini mwa nchi hiyo.
Hii ndi kwa sababu Marekani imeona Uturuki kuwa nchi mwafaka katika kufanikisha sera yake mpya kwa suala la siasa za Mashariki ya Kati.
Uturuki pamoja na Urusi wakishirikiana na Iran amefanya juhudi na kufanikisha usitishaji wa vita Syria vilivyoendelea kwa muda wa miaka 6 , baada ya hapo awamu za kwanza na pili za mazungumzo ya Astana pia zimepita kwa mafanikio kwa ajili ya juhudi na sera nzuri walizotumia kuhusu suala hilo.
Wiki za hivi karubuni kumekuwa na misururu ya ziara za viongozi wa kimataifa jijini Ankara kama Theresa May, Angela Merkel na Antonio Guterres ishara ya kuwa sasa Uturuki inaonekana kuwa kituo muhimu kwa masuala ya kimataifa .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment