Image
Image

Madaktari wafanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa kubadilisha mlango wa moyo.

MADAKTARI wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza  wamefanya upasuaji mkubwa wa kubadilisha milango zaidi ya miwili ya moyo iliyokuwa imeziba.
Upasuaji huo  umefanywa na madaktari hao kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya   Mumbai,   India.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji JKCI, Bashir Nyangasa alisema kambi ya upasuaji ilianza Machi 26  mwaka huu na kumalizika jana.
“Tumefanya pia upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika milango ya moyo iliyokuwa imeziba. 
Upasuaji huu kitaalamu unaitwa ‘Coronary Artery Bypass Graft’. Tumewafanyia   wagonjwa wanane,” alisema.
Alisema wamemfanyia upasuaji mtoto wa umri wa miaka minane ambaye mshipa wake mmoja ulikuwa umesinyaa.
Naye  Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa JKCI,Dk.Peter Kisenge alisema kwa mara ya kwanza waliweza kuzibua mlango wa moyo ambao hupitisha damu isiyo na hewa ya oksijeni kuipeleka kwenye moyo, ambao ulikuwa umeziba.
“Tumewafanyia upasuaji bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa ‘cath lab’ wagonjwa 12 ambao mishipa yao iliziba kwa asilimia 100. Mgonjwa mmoja tumemuwekea betri ya pacemaker,” alisema.
Alisema tangu Januari  mwaka huu hadi Machi, taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa nje ya nchi, imefanya upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 79.
“Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje,Serikali ingetumia   Sh bilioni 2.1 na kila mmoja angegharimu zaidi ya Sh milioni 27,” alisema.
Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani, Mtakatifu Dk. Syedna Aliqadr Mufaddal alipokutana na Rais Dk. John Magufuli Oktoba, mwaka jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment