Image
Image

Abe alaani vikali shambulizi la bomu lililotokea katika njia ya treni jiji la St. Petersburg.

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amelaani vikali shambulizi la bomu lililotokea katika njia ya treni ya chini ardhi ya jiji la St. Petersburg na kuelezea dhamira yake ya kupambana na ugaidi kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Waziri Mkuu Abe alizungumza na waandishi wa habari hivi leo 04 April 2017 na kutoa rambirambi zake kwa familia za waliopoteza ndugu zao pamoja na majeruhi wa shambulizi hilo.
Amesisitiza kuwa vitendo vya ugaidi kamwe haviwezi kuvumiliwa na kwamba Japani ipo pamoja na Rais Vladimir Putin na watu wa Urusi katika kipindi hiki kigumu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment