Image
Image

Rais Magufuli kuwaapisha wateule 8 wa kamati ya pili ya uchunguzi wa Madini Ikulu.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo 11 Aprili, 2017 anawaapisha wajumbe wanane wa kamati maalum ya pili itakayo fanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wajumbe hao waliteuliwa 10 Aprili 2017, Kamati hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamatiya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi iliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwani;
1. Prof. Nehemiah EliachimOsoro
2. Prof. Longinus KyaruziRutasitara
3. Dkt. Oswald Joseph Mashindano
4. Bw. Gabriel Pascal Malata
5. Bw. Casmir Sumba Kyuki
6. Bi. ButamoKasuka Philip
7. Bw. UsajeBenardUsubisye
8. Bw. Andrew Wilson Massawe
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment