Image
Image

Tanzania yapanda nafasi ya 135 kwenye viwango vya ubora wa soka vya FIFA.

Katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA leo Aprili 6, 2017 Vimeonesha kuwa Tanzania imepanda kwa nafasi 22 hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 kati ya mataifa 211 .
Siku za usoni Tanzania katika mechi za kalenda ya FIFA, iliwashinda Botswana na Burundi katika michezo miwili tofauti zilizofanyika Machi, mwaka huu.
Katika viwango hivyo vipya vya mwezi April, Brazil imeishusha Argentina kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Argentina ikishuka hadi nafasi ya pili na Ujerumani imebaki katika nafasi yake ya 3.
Katika ‘top ten’, mataifa yanayofuata ni Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswisi na Hispania inakamata nafasi ya 10
Barani Afrika Misri  inaongoza ikiwa nafasi ya 19 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 30, Cameroon nafasi ya 33,  Burkina Faso nafasi ya 35, Nigeria nafasi ya 40 na Congo DR nafasi ya 41 ikiwa mbele ya Tunisia kwa nafasi moja
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda bado inaongoza ikiwa imepanda kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 72, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117,  Ethiopia nafasi ya 124, Tanzania nafasi ya 135 na Burundi imeshuka kwa nafasi mbili hafasi ya 141.
Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 194 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment