Image
Image

Rungu aliloshushiwa mdee kutohudhuria vikao vya bunge lamgusa Zitto,Mbowe, Bulaya waonywa.

Kamati ya Bunge imetoa adhabu kwa Mbunge wa Kawawe Halima Mdee (CHADEMA) ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobaki kutokana na siku za usoni kutoa lugha ya matusi Bungeni.
Halima mdee alitoa lugha hizo za matusi siku za usoni ndani ya bunge  zikiwahusisha Spika wa bunge hilo Mh.Job Ndugai na Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangallah, lakini aliweza pia kuomba radhi wahusika na bunge kwa ujumla.
Kutokana na taarifa ya Kamati ya Bunge juu ya kumsimamisha Mdee vikao vilivyobaki baadhi ya wabunge akiwamo Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe(ACT) amelani na kuandika machache kupitia ukurasa wake wa Twitter.
"Sio HAKI. @halimamdee kaomba radhi ndani ya Bunge, kwanini aadhibiwe tena? Huyu ni Waziri Kivuli Fedha, mwaka wa pili Sasa anakosa Bajeti."Amesema Zitto Kabwe.
Mbali na kamati hiyo ya bunge kutoa adhabu kwa mbunge wa kawe, pia imemsamehe Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau muhimili huo wa Bunge April 4, 2017, huku ikimuonya Mbunge mwingine ni Ester Bullaya baada ya kukiri kosa lake lakutoa lugha za kuudhi ndani ya bunge hilo.
                                                    Freeman Mbowe -CHADEMA.
                                                   Ester Bulaya - CHADEMA
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment