Image
Image

Tanzia:Mwanamuziki wa nyimbo za dansi Shaban Dede afariki Muhimbili.

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za dansi nchini Tanzania Shaban Dede aliyekuwa kalazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari amefariki amefariki asubuhi ya 06 Julai 2017.
Kwa taarifa za awali nikwamba ndugu pamoja na mwanae wapo hospitali ya Muhimbili kupata utaratibu baada ya kutokea msiba wa mpendwa wao, kisha ndipo waweze kuona ninamna gani wanaweka mipango sawa ya mazishi kisha maziko.
Jina la Shaban Dede si geni kwa watu ambao wamekuwa wakifuatilia muziki ambapo angu miaka ya sabini na ameshawahi kufanya kazi katika bendi mbalimbali maarufu zilizokuwa zikitamba miaka hiyo.
HISTORIA YAKE KIKAZI.
“Nimezaliwa Mkoa wa Kagera 1954. Nilianza kupenda muziki nikiwa bado mdogo kabisa na bendi yangu ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni ya TANU ambayo makazi yake yalikuwa Biharamulo, Bukoba.
“Mwaka 1974 nilijiunga na Bendi ya Polisi na mwaka 1975, nikajiunga na Tabora Jazz napo nilikaa kidogo, 1976 nilihamia Dodoma Internationl Band ambapo nilidumu kwa miaka mitatu.
“Ulipofika mwaka 1979 nilienda Msondo ambapo nilifanya kazi hapo mpaka 1982 nikahamia Mlimani Park, hapo nilikaa mwaka mmoja nikaenda Bendi ya Bima na mwaka 1987 nilirudi Msondo ambapo napo nilikaa kidogo nikahamia Sikinde kisha nikarudi Msondo 2011 mpaka leo niko hapo.
NINI KILIMFANYA KUHAMA BENDI KILA MARA?
“Unajua zamani tulipokuwa tunachipukia, tulikuwa tunaangalia wapi upepo unapoangukia na pia kutafuta masilahi zaidi lakini kwa sasa mtu huwezi kuhamahama.
KITU GANI KINACHOFANYA MUZIKI WA DANSI KUDUMAA?
“Muziki wa dansi ulikuwa juu sana zamani lakini ulidumazwa na vyombo vya habari viliupa kisogo kabisa muziki huu maana hata redioni tunasikika kwa nadra sana kitu ambacho siyo sahihi, kitu kingine chama chetu cha Mapinduzi kimeuporomosha sana muziki huu kwa sababu mara nyingi hata kwenye kampeni wanawatumia vizazi vipya.
ANAONGELEAJE MUZIKI WA KIZAZI KIPYA?
“Wanamuziki wa Kizazi Kipya  wanafanya vizuri lakini kuna nyimbo nyingine ambazo zinavunja maadili kabisa, kwa mfano mimi nampongeza Diamond kwa nyimbo zake lakini kuna nyimbo yake moja sivutiwi na maneno yake maana kuna sehemu anaimba “kidonda chako kwangu maradhi” hii huwezi kuimba mbele ya mzazi.
“Nawaomba waimbe nyimbo na watumie maneno kwa tafsida ili hata watu waweze kuziimba kwa heshima.
NINI KERO YAKE KWENYE BENDI?
“Kero kubwa kwa wanamuziki wa bendi nyingi nilizopitia ni husuda, kuamini ushirikina maana mtu anaweza akakusema wewe mchawi sasa unajiuliza amejuaje kuwa wewe ni mchawi kama na yeye si mtu wa kupita kwa waganga?
MAFANIKIO KWENYE MUZIKI
“Unajua faida niliyopata kwenye muziki inaenda na vipengele. Mfano enzi zile za Nyerere (hayati Julius Kambarage) niliweza kununua baiskeli, kipindi cha Mwinyi (Ali Hassan) nilinunua DCM na mpaka sasa nimeweza kupata nyumba kubwa ya kuishi ndiyo hasa kitu nilichofaidika nacho.
KUHUSU FAMILIA
“Nina mke naishi naye na nimejaaliwa kupata watoto watano.
KUNA MTOTO AMEFUATA NYAYO ZAKE?
“Labda huyu mdogo lakini wengine wote naona wamevutiwa zaidi na wanachokifanya lakini huyo mdogo kama ataendeleza kipaji chake nitampa sapoti kubwa kwa kuwa muziki wa vijana sasa hivi una kipato kikubwa sana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment