Image
Image

LUKUVI atoa agizo kwa Maafisa Mipango Miji kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao



Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipango Miji kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki zao za ardhi kwa dhuluma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI ametoa agizo hilo  Wilayani SUMBAWANGA Mkoani RUKWA alipoenda kutatua mgogoro wa ardhi, kuwa tatizo la ujenzi holela linachangia migogoro ya ardhi.
Katika hatua nyingine, Waziri LUKUVI ameagiza eneo lililokuwa shamba la mifugo la MALONJE Wilayani SUMBAWANGA lenye ukubwa wa zaidi ya Ekari Elfu Kumi na Mbili lirejeshwe serikalini kwa vile utaratibu wa kuligawa umekiukwa huku masharti ya uendeshaji yakiwa hayajazingatiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment