Image
Image

CIA yatoa faili 470,000 zilizopatikana wakati wa kuuawa kwa Osama Bin Laden.

Shirika la ujasusi la Marekani CIA limetoa karibu faili 470,000 zilizopatikana wakati wa kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden mwaka 2011.
Faili hizo mpya ni pamoja na stakabadhi kuhusu mipango yake binafsi na video ya mtoto wake wa kiume Hamza wakati wa hasuri yake.
Hii ndiyo mara ya nne CIA inatoa faili za Osama zilizopatikana wakati wa uvamizi kwenye maficho yake huko Abbottabad nchini Pakistan.
Hata hivyo faili zingine haziwezi kutolewa kwa sababu zinaweza kuathiri usalama wa tiafa.
Kulingana na CIA faili hizo zinafichua uhusiano uliopo sasa kati ya al-Qaeda na ISIS na migawanyiko kati ya al-Qaeda na washirika wake.
Kampiuta iliyopataiaka wakati wa uvamizi huo ilikuwa na filamu za Hollywood, vipindi vya watoto na makala tatu kumhusu Osama Bin Laden.
Video nyingine ni ya harusi na mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden akiwa mdogo. Hamza Bin Laden sasa ana umri wa miaka ya 20 licha ya mahali aliko sasa kutojulikana.
Stakabadhi za awali zilionyesha kwa Bin Laden alikuwa akimundaa mtoto wake huyo kumridhi kama kiongozi wa al-Qaeda.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment