Image
Image

Maghorofa ya Lugumi kuuzwa kesho


Kampuni ya Udalali ya Yono kesho itaziuza kwa mnada nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi.

Mnada huo wa kesho Alhamisi Novemba 9,2017 unafanyika kwa mara ya pili baada ya wa kwanza wa Septemba 7,2017 kukwama kutokana na wateja waliojitokeza kutofikia bei iliyohitajika.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Novemba 8,2017 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Scholastica Kevela amesema, “Mnada huo upo kama tulivyotangaza na utafanyika kesho asubuhi hivyo wanaohitaji wajitokeze kwa wingi."
Amesema lengo la mnada huo ni kufidia Sh14 bilioni ambazo mfanyabiashara Lugumi anadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Scholastica amesema bei ya kila nyumba itatangazwa eneo husika na wote wanaozihitaji wawe kutoka ndani au nje ya nchi wanakaribishwa.
Nyumba mbili kati ya tatu ambazo zitapigwa mnada ziko Mbweni JKT na nyingine Upanga, jijini Dar es Salaam.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment