Image
Image

Ofisa mtendaji mkuu wa Acacia na ofisa mkuu wa fedha wamejiuzulu.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon na ofisa mkuu wa fedha Andrew Wray wamejiuzulu, kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini imetangaza leo.
Kampuni hiyo yenye migodi mitatu ya dhahabu kaskazini magharibi mwa Tanzania imetangaza kuwa wawili hao wataondoka rasmi Acacia mwishoni mwa mwaka huu. Hata hivyo, taarifa inayopatikana kwenye tovuti ya kampuni imeeleza kuwa, Peter Geleta ataiongoza kampuni hiyo katika kipindi cha mpito huku Jaco Maritz akiongoza kitengo cha fedha.
Wateule hao wataanza kazi kuanzia Januari 1, mwaka kesho, akizungumzia kujiuzulu kwa Brad na Andrew, mwenyekiti wa Acacia, Kelvin Dushnisky amenukuliwa na taarifa hiyo akisema, “Brad na Andrew wamekuwa kiungo muhimu katika uendeshaji na masuala ya fedha hapa Acacia kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne.
Kwa niaba ya bodi, ninapenda kuwashukuru kwa mchango wao kwenye kampuni. Tunawatakia kila la heri kwa siku za usoni.”
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment