Image
Image

Wanajeshi 18 wa Malawi wamefariki baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuacha njia.

Wanajeshi 18 wa Malawi wamefariki dunia baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuacha njia kwenye kona na kuvingirika mara tatu.
Lori hilo la Jeshi lilikuwa limewabeba abiria 60 wakirejea kut o ka kwenye mafunzo katika Wilaya ya Mzimba.
Msemaji wa Polisi wa Wilaya ya Mzimba,Bwana PETER BOTHA amethibitisha vifo vya watu hao 18 ambao ni pamoja na dereva wa lori hilo na wakufunzi watatu.
Amesema majeruhi kadhaa wamelazwa katika hospitali iliyopo jirani na eneo la tukio.
Wakati huo huo Mahkama nchini Malawi imewatia hatiani watuhumiwa watatu kwa kufukua kaburi la msichana aliyekuwa na umri wa miaka 16 aliyekuwa Albino kwa Imani za ushisrikina.
Watuhumiwa hao THOMAS NDINI, ENOCK BANDA, na JONAS OGARA,wametiwa hatiani kwa kufukua kaburi la mwili wa  CHOSADZIWA KAUNDA kinyume cha sheria.
Hukumu ya watu inatarajiwa kutolewa tarehe 17 mwezi huu.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment