Wanafunzi Chuo kikuu UDSM wakimsikiliza bigwa wa uchumi kutoka nchini Idia. |
Tanzania inaweza kupiga hatua za kimaendeleo na kiuchumi kwa
kutumia rasilimali zake zilizopo nchini, ikiwa katika kupanua na kuwekeza katika elimu ya juu ikiwemo ya biashara, na
Kusimamia vyema wawekezaji katika sekta mbali mbali.
Hayo yamebainishwa na
Profesa Swami Partasaraty, bingwa wa kimataifa wa uchumi kutoka nchini india ,
alipo kuwa akitoa mhadhara kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha biashara jijini Dar
es Salaam ambapo amesema kuwa nchi zinazofanikiwa ikiwamo india zimekuwa
zikisimamia vyema sera za uwekezaji pamoja na kujikita katika utafiti ambao kwa
kiasi kikubwa imeweza kusimamia uchumi wake bila kutegemea nchi wahisani.
0 comments:
Post a Comment