Image
Image

VIONGOZI WATAKIWA KUWA WABUNIFU

Viongozi mbalimbali nchini wamekumbushwa kuwa wabunifu katika kutatua matatizo ya wananchi ili kuhakikisha wanakabiliana  kero za wananchi wanaowaongoza.

Hayo yamesemwa na mbuge wa ilala Mussa Zungu wakati wa uzinduzi wa daraja la muda katika kata ya ilala na bunguruni mapema leo ambapo amesema kutokana na ufinyu wa bajeti ya halmashauri kuweza kujenga daraja la kudumu hivyo wameamua kuweka daraja la muda kwajili ya kuwasaidia wananchi kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi hao.
Mussa  Zungu...Mbunge wa ilala
Aidha Zungu amesema daraja hilo la muda litakamilishwa hapo badae kwajili ya kujengwa kwa uimara zaidi na kufanya kuwa liwe la kudumu.

Kwaupande wao  wakazi wa kata ya ilala  wamesema kabla ya daraja hilo kujengwa walikuwa wakipata adha kubwa sana katika kuvuka kutoka upande mmoja kwenda wa pili hivyo kwasasa wamepata daraja hilo la muda ambalo limewarahisishia katika kuvuka .

Daraja hilo ambalo ni mkombozi wa kwa wakazi wa ilala na bunguruni limegharimu jumla ya shilingi milioni mbili na nusu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment