Image
Image

CHAMA CHA CUF CHATOA ONYO KWA SERIKALI.

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeionya Serikali kutotekeleza azma ya kuwakamata viongozi wa chama hicho kwa kuwahusisha na vurugu zilizotokea mkoani Mtwara hivi karibuni, kwa maelezo kuwa hatua hiyo, haitosaidia kumaliza mgogoro huo.
Kauli hiyo ya CUF, ambayo imetolewa leo, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, imekuja siku chache baada ya kutokea kwa vurugu mkoani Mtwara zilizotokana na shinikizo za wananchi kupinga uamuzi wa Serikali wa kusafirisha gesi kutoka mkoani humo.
Mwenyekiti wa chama hicho cha  Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, akiwaonesha waandishi wa habari, taarifa iliyotolea na Ikulu kuhusu kupatikana kwa mwekezaji kwenye masuala ya mradi mkubwa wa umeme, uliokuwa ukitaka kujengwa mkoani Mtwara na kisha Profesa Lipumba kuwaelezea waandishi wa habari kuwa mradi huo haukutekelezwa tena na hivyo kusema hayo nimoja ya masuala yaliyokuwa yakiwaweka wananchi wa Mtwara katika sintofahamu ya hatima ya mategemeo yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.  Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo na kulia ni Ofisa Utawala wa CUF, Twaha Rashid.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, akielezea jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, na  Kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana CUF Taifa, Katani Katani.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam, kuhusu ghasia zilizofanywa na baadhi ya wananchi wa Mtwara hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, CUF imepata taarifa kuwa Serikali imepanga njama za kuwakamata wanasiasa mbalimbali wakiwamo viongozi wa chama hicho, wakiwahusisha na vurugu hizo.
Alisema kuwa kitendo hicho, hakitokuwa sahihi kwa kuwa wanasiasa hawahusiki na vurugu hizo na kwamba hakitovumiliwa kamwe.
"Tumepata taarifa za kuaminika kuwa Serikali inapanga kukamata viongozi wa siasa wakiwamo wa CUF, kuwahusisha na yaliyotokea Mtwara, sisi kama CUF tunaimabia Serikali kuwa hilo si jambo sahihi na si kweli kama wanasiasa wanahusika, wasitafute mchawi katika hilo," alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, aliitaka Serikali kuruhusu wanasiasa kwenda mkoani Mtwara kwa kuwa siasa ndio jambo litakaloweza kusaidia kumaliza mvutano huo, baina ya Serikali na wananchi.
Alisema kitendo cha kuzuia kufanyika mikutano ya kisiasa hakitosaidia kumaliza mgogoro huo na kwamba nguvu ya siasa na ushawishi wa kisiasa unaweza kusaidia kumaliza mvutano huo.
"Wanasiasa wanahitajika Mtwara kufanya siasa, ili kumaliza kashikashi iliyopo mkoani humo, Serikali inatakiwa ikubali hilo na iruhusu tukafanye mikutano ya kuwaelimisha wananchi wa Mtwara," alisema Profesa Lipumba.
Mbali na hilo, Profesa Lipumba alilitaka Bunge kuunda kamati maalumu ya kufuatilia kwa kina sakata hilo, la gesi ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa jambo ilo.
Alilitaka Bunge pia kuhoji matumizi ya sh. milioni 540, ambazo katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012, ilitengwa kutekeleza mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia eneo la Mnazi Bay, mkoani Lindi.
Profesa Lipumba alilaani matumizi ya nguvu katika kudhibiti vurugu hizo na kusema kuwa Serikali inapaswa kutafuta ufumbuzi wa chanzo cha vurugu hizo na si kushughulikia matokeo yake.
Alisema Serikali inapaswa kutekeleza miradi iliyoahidi kuitekeleza katika mkoa Mtwara, na kuacha maneno ya siasa bila vitendo na kupandikiza chuki kuwa watu wa Mtwara ni wachoyo wa rasilimali.
Aliongeza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ikiwamo ujenzi wa kiwanda cha Mbolea pamoja na vinginevyo, kutamaliza mvutano uliopo sasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment