Image
Image

EXCLUSIVE: MCT YASEMA HAITOTETEREKA DHIDI YA KAULI YA NKAMIA ALIYOITOA BUNGENI KWANI HAYANA UKWELI WOWOTE MADAI YAKE.

Baraza la habari Tanzania MCT limesema halitatetereka katika jukumu lake la kusimamia weledi, maadili na maendeleo ya waandishi wa habari nchini licha kile lilichodai kushutumiwa bungeni hivi karibuni na mbunge mmoja kuwa ni shirika lisilo la kiserikali ambalo halifanyi kazi ya habari.
JUMA NKAMIA - MBUNGE WA KONDOA KUSINI


Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa baraza hilo Kajubi Mukajanga amedai kuwa madai yaliyotolewa na mbunge wa Kondoa Kusini  Juma Nkamia wakati akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo hayana ukweli, yanapotosha umma na kurudisha nyuma juhudi ya baraza hilo katika maendeleo ya tasnia ya habari hapa nchini.
KAJUBI MUKAJANGA - KATIBU MTENDAJI MCT
Aidha amesema baraza hilo lenye wanachama zaidi ya 130 zikiwemo taasisi na vyombo vya habari limeanzishwa kwa nia njema pia limekuwa likisaidia kuleta usuluhishi kati ya vyombo vya habari na hata viongozi wakuu wa serikali kupitia kamati yake ya maadili ambayo inaongozwa na jaji mstaafu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment