Rais mstaafu Alhaji Ali
Hassan Mwinyi amesema suala la
mmomonyoko wa maadili, kupotea kwa umoja na misingi ya jadi na ujamaa kutokana
na kuwepo kwa ubinafsi katika jamii kumechangia taifa kupoteza mwelekeo wake
katika suala zima la kuwasaidia wazee wasiojiweza hususan wanaoishi maeneo ya
mijini.
 |
ALHAJI ALI HASSAN MWINYI-Rais Mstaafu Tanzania |
Alhaj Mwinyi ametoa kauli
hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa
makazi ya wazee jijini Dar es Salaam yatakayogharimu shilingi milioni 300.
Amesema kukithiri kwa
ubinafsi miongoni mwa wananchi kumesababisha wazee kukosa huduma muhimu ikiwemo
malazi, mavazi, huduma za afya pamoja na chakula cha uhakika na hivyo wengi wao
kuamua kukimbilia mitaani na kugeuka kuwa ombaomba.
 |
ALHAJI ALI HASSAN MWINYI- Rais Mstaafu Tanzania |
Ameyaomba mashirika na watu
binafsi kuunganisha nguvu zao na kujitoa kwa hali na mali katika kuchangia
maendeleo ya wazee kwani wazee ni
rasimali, kielelezo cha hekima bora na ngao kwa taifa na kwamba taifa lisilothamini
wazee ni sawa na kupoteza historia, mila
na utamaduni wake.
 |
BALOZI JUMA MWAPACHU -
AKISIKILIZA KINACHOENDELEA KWENYE MKUTANO HUO.
|
Awali Mwenyekiti wa Taasisi
ya Tushikamane Bi Rose Mwapachu na mlezi wa asasi hiyo Bi Aisha Bilal walisema
kwamba asasi hiyo imekwishawafikia wazee 36 jijini Dar es Salaam tangu kuanzishwa kwake ambapo
wamekuwa wakitoa misaada ya kibinadamu ikiwemo lishe, mavazi na huduma za afya
kila mwezi.
 |
ROSE MWAPACHU - Mkiti TPF |
 |
AISHA BILAL - Mlezi TPF |
 |
WADAU MBALI MBALI WAKITETA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment