Mwambusi
amesema kuwa makocha wa Simba wamehangaika sana kutafuta
wachezaji wa kucheza nafasi ya ulinzi ili kuziba pengo la baadhi ya wachezaji
waliotimka Msimbazi akiwemo beki wa kati wa Yanga Kelvin Patrick Philip Yondan
aliyeihama Simba mwishoni mwa msimu wa mwaka jana.
Kocha
huyo aliyekuwepo uwanja wa taifa hapo jana kushuhudia mtanange huo uliovuta
hisia za mashabiki wengi nchini Tanzania amesisitiza kuwa bao la kwanza la
Yanga lilifungwa baada ya mabeki wa Simba kushindwa kukaba vizuri na kujua wapi
mpira utatua.
“Kipa
Juma Kaseja aliwapanga mabeki wake upande wa kulia kwake na mpira ulitua kule,
lakini akasahau upande wa kushoto ambao angekaa yeye, angalia Kavumbagu
alivyopiga kichwa chepesi na kuingia katika kona ya goli ambapo hakukuwa na
mlinzi yeyote, lile ni kosa kubwa”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi
aliyesisitiza kuwa jana alilazimika kufika uwanjani ili kujifunza zaidi kuliko
kutazama mpira kama shabiki wa kawaida aliongeza kuwa hata bao la pili la Hamis
Kiiza lilitiwa kambani kufuatia uzembe wa mabeki wa Simba kushindwa kuosha
mpira wa kona langoni kwao.
“Sisi
walimu huwa tunawafundisha wachezaji kuwa lazima beki aangalie mpira utatua
wapi na jinsi wachezaji wa timu pinzani alivyokaa (watch the ball, watch
the opponent players movement) , wakati kona inapigwa mabeki wa Simba
hawakuangalia wachezaji wa Yanga wamekaa vipi na hatari iko wapi, mpira
ulimkuta sehemu nzuri Kiiza na kufunga bao rahisi”. Alisema kitaalamu Mwambusi.
Kocha
huyo aliendelea kueleza kuwa walinzi wa Simba wanaocheza nafasi hiyo kiukweli
asili yao siyo mabeki.
“Muangalie
Kapombe ambaye ni kiraka, anachezeshwa sehemu ya beki wa kati wakati yeye
anafanya vizuri zaidi pembeni, hata Musa Mude ni kiungo, lakini mwalimu
kalazimika kumchezesha nafasi ya ulinzi, ukiwaangalia mara nyingi wanakosa
mawasiliano mazuri na ndio maana jana wamepoteana sana”. Alisema Mwambusi.
Akizungumzia
kikosi cha Simba, Mwambusi alisema watu wengi waliibeza klabu hiyo, lakini yeye
ameona kuwa Simba ina wachezaji bomba ambao kama watatunzwa msimu ujao wa ligi
watakuwa na timu bora zaidi.
“Wachezaji
vijana wamefanya kazi nzuri sana na wanaonekana kuwa makini na kutulia sana,
wakiendelea kuwa pamoja na kucheza kwa muda mrefu, Simba itakuwa tishio”.
Alisema Mwambusi.
Mwambusi
alisema Simba kwa sasa bado ina matatizo na haijatengamaa ukilingaisha na msimu
uliopita, na hii inatokana na kushindwa kupata wachezaji mbadala wa baadhi ya
nyota wake waliotimka.
“Pengo
la Yondan bado lipo, Emmanuel Okwi, ma Marehemu Patrick Mafisango, hakika
kukosekana kwa wachezaji hawa imekuwa tatizo kubwa kwa Simba, nadhani timu ipo
wakati wa mpito na itawahitaji kutulia na kutengeneza kikosi chake”.
Alisema mechi ya jana imempa nafasi ya kujua falsafa za Soka la Simba na Yanga
hata kama wanaweza kubabili, hivyo inampa changamoto ya nini cha kufanya akiwa
na kikosi chake cha Mbeya City msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment