Image
Image

Misri yakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na utekaji huko Sinai


Serikali ya Misri imewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na kutekwa nyara kwa askari 7 katika eneo la Green Valley, kaskazini mwa Sinai.
 Askari hao waliachiwa tarehe 22, Mei, siku sita baada ya kutekwa. 

Watuhumiwa hao wamekamatwa jana mjini Arish, na wanatuhumiwa kuhusika na kutuma video ya askari waliotekwa nyara kwenye mtandao siku mbili baada ya askari hao kutekwa. 
Mohamed Morsi - Rais Misri.
Video hiyo inawaonyesha askari hao wakimtaka Rais Mohamed Morsi wa Misri kutekeleza masharti ya watekaji hao ambao walimtaka rais huyo kuwachilia ndugu zao walioko gerezani kutokana na kuhusika na mashambulizi ya kigaidi. 
 
Msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine wa tukio hilo bado unaendelea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment