Image
Image

Zimbabwe yasema ziara ya rais Mugabe nchini Japan ni dalili ya kuvunja ukimya


Shirika la habari la Zimbabwe New Ziana limesema, ziara ya rais Robert Mugabe wa nchi hiyo nchini Japan ni dalili kuwa nchi hiyo inaanza kutoka kwenye kipindi cha kutengwa na nchi za magharibi.
ROBERT MUGABE
Shirika hilo limesema, rais Mugabe atahudhuria mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika utakaofanyika Yokohama jumamosi hii. Hii ni mara ya kwanza kwa Zimbabwe kuhudhuria mkutano huo tangu uanzishwe mwaka 1993.

Rais Mugabe ambaye yuko kwenye orodha ya Marekani na Umoja wa Ulaya ya watu waliowekewa vikwazo, anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ambapo pia ni mara ya kwanza kwa rais huyo kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi wa nchi kubwa inayoegemea nchi za magharibi. 

Viongozi wa Zimbabwe na Japan walikutana kwa mara ya mwisho mwaka 1989.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment