Serikali imetenga
Sh.bilioni 9.8 kwa ajili ya mikopo ya vifaa kwa
wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuboresha uchimbaji wao na
watakopeshwa
kupitia vikundi watakavyojiunga na itakuwa mkopo endelevu
ili kuinua
sekta hiyo ya madini kupitia wachimbaji hao.
Hayo yamezungumzwa na Kamishna wa madini wa kanda ya kaskazini
Eng.Benjamini Mchwampaka wakati wa mahojiano na
waaandishi wa habari
yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko
mkoani arusha.
Amesema kuwa kupitia
mikopo hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa
wachimbaji
hao kupata vifaaa hivyo ili kuweza kuinua uchimbaji wao na
kuwa wa
kisasa zaidi ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini ambapo
hivi sasa
wamekuwa wakikwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa hali
ambayo
wanachimba ila hawapati madini ya kutosha.
Ameongeza kuwa wachimbaji
wadogo wa kanda ya kaskazini bado
wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali katika uzalishaji madini
ikiwemo
kutokuwa na vifaa vya uchimbnaji vya kisasa ,bei kubwa ya
milipuko
na elimu ndogo ya uchimbaji madini hayo hali ambayo
inakwamisha
jitihada zao za kuchimba madini hayo na kuwarudisha nyuma
katika
kujikwamua kiuchumi
Alisema kuwa hivi sasa wachimbaji wadogo walio wengi
wanachimba kwa
mazoea na vifaa duni ambapo elimu ya utambuzi madini
sehemu yalipo ni
ndogo hali ambayo inasababisha kutopata madini
yakutosha na kutumia
gharama kubwa zaidi.
Eng.Mchwampaka alisema
kuwa katika kanda hii wachimbaji wamekuwa
wakichimba kiholela bila lessen hali ambayo inaweza
kuhatarisha
usalama wa maisha yao na hata kusababisha kifo na madhara
mbalimbali
ambapo maeneo hayo yanachimbwa kwa kesi sana hali
ambayo ni hatari
kwa badala yake wachimbaji wafate taratibu za
kuchimba eneo tengefu
kwa madini kwa maendeleo yao na usalama wa maisha
yao kuepuka kupoteza
nguvu kazi ya taifa.
Aidha aliongeza kuwa
hivi sasa ofisi ya kanda imejiwekea mkakati
mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma karibu na
wachimbaji katika kanda
hii
hususan kutoa elimu ,ya uchimbaji wa madini kitaalamu zaidi,hali
ya
masoko ,afya migodini ,ajira na kutoa mafunzo kwa vitendo ya namna
ya
ulipuaji mogodini sambamba na watatoa fursa ya namna ya uchimbaji
salama
na wenye tija na maendeleo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Eng.Mchwampakka alisema kuwa hivi sasa wako kwenye mchakato wa
kuandaa
maonyesho ya vito ,na
madini mbalimbali yatakayofanyika oktoba 28hadi 30 mwaka huu mkoani hapa
ambapo watahiusisha wafanyabiashara
wote ncnini na nchi jirani
ikiwemo Kenya ,DRC kongo ,Zambia ,Madagascar
,Malawi ,Ethiopia ,Afrika
ya kusini na Msumbiji ili kuweza
kubadilishana uzoefu na kuweza kuongeza
ushindani katika sekta ya
madini nchini.
0 comments:
Post a Comment