Wakazi wa Kigamboni
wilayani Temeke wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kuwaamini watendaji wake
kuwa suala la wakazi la kupinga kuondoka katika eneo hilo kupisha ujenzi wa mji
wa kibiashara limekwisha.
Wakizugumza kwa nyakati
tofauti kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya
Serikali ya Mtaa wa Kifurukwe kata ya Kibada jijini Dar es Salaam jana, wakazi
hao zaidi ya 300 walisema kuwa hawako tayari kuondoka katika eneo hilo kwa
gharama yeyote hata kama ni kumwaga damu wako tayari.
Walisema suala hilo la
kupisha ujenzi mpya wa jiji la kigamboni halijakwisha kutokana na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Makazi kuliendesha kinyume cha sheria na propaganda.
Mwenyekiti wa Mkutano huo,
Issaya Mathayo alisema wakazi hao hawana nia ya kumwaga damu ya mtu bali
wanaitaka serikali kuwa makini ili kuepuka kuufikisha mgogoro huo katika hatua
hiyo.
“Mnajua suala la ardhi
si la mchezo mchezo kuitoa ni rahisi lakini kuipata tena gharama yake ni kubwa
hivyo tunaahidi hakuna atakaye ondolewa kirahisi pa ieleweke kuwa hatupingi
maendeleo kikubwa sheria zitumike”alisema Mathayo.
Mathayo alisema
kinachosikitisha hadi sasa hakuna mchakato wa kueleweka wa tathimini za
mali zao iliyofanyika kwa ajili ya fidia.
Aidha, kuanzia jana
wameamua kuicha kamati ilioundwa kwa ajili ya kusimamia maslahi yao kutokana na
kamati hiyo kuwa upande mmoja na serikali.
Naye Mwalami Mwinyimvua,
alisema mradi huo wananufananisha na ule wa makongo, kwamba ule mbona hauna
manung’uniko ni kutokana na mradi huo kuendeshwa kwa kuzingatia sheria katika
mali za wananchi husika.
Alisema tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 2008 ieleweke
kuwa hakuja kuwa na makubaliano yeyote kati ya serikali na wananchi hao
kinachoendelea ni propaganda katika vyombo vya habari vya serikali.
Mwinyi aliwalaumu madiwani
wote wa Jimbo la kigamboni kushindwa kuwatetea wakazi hao katika kujua hatima
yao na baadala yake wamejiingiza kwenye kazi ya udalali wa vinja kwa maslahi
binafsi.
0 comments:
Post a Comment