Image
Image

BAADA YA HALI YA MZEE MANDELA KUZOROTA KWA SAA 48, RAIS JACOB ZUMA ASITISHA ZIARA YAKE NCHINI MSUMBIJI.


Hali ya rais wa zamani wa Afrika kusini Mzee Nelson Mandela imeripotiwa kuzidi kuzorota katika saa 48 zilizopita hatua iliyomlazimu rais Jacob Zuma wa nchi hiyo kufuta ziara yake ya kwenda Msumbiji ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais uliokuwa umepangwa kufanyika leo.
Nelson Mandela - rais wa zamani wa Afrika kusini 
Habari kutoka nchini Afrika Kusini zinasema, rais Zuma amefikia uamuzi huo baada ya kumtembelea Mzee Mandela kwenye hospitali alikolazwa kwa ajili ya matibabu na kuelezwa na madaktari wanaomhudumia kwamba hali yake imezidi kuzorota hali inayozua taharuki zaidi nchini humo.
Jacob Zuma - Rais wa Afrika Kusini 
Watu mbalimbali wameendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Mzee Mandela wakiwa na ujumbe wa kumtakia heri kiongozi huyo anayeheshimika duniani na kwa mujibu wa wadadisi wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.




Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment