Mabomba ya mradi huo wa bomba Gesi yakiwa Kwenye Gari.
|
Waziri mkuu Mizengo Pinda
amewataka wadau mbalimbali nchini kuwa wajumbe wa kutoa elimu kwa wananchi ili
kuwaongezea uelewa kuhusiana na mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka
Mtwara na Songosongo hadi Dar es salaam na kutoa ushirikiano ili kuwezesha
utekelezaji wa mradi huo wenye manufaa makubwa kwa taifa.
Mizengo Pinda - Waziri Mkuu Tanzania |
Shehena ya mabomba kwaajili ya ujenzi wa Bomba la gesi ukionekana hapo. |
Waziri mkuu ameyasema hayo
katika hafla ya kupokea shehena ya kwanza ya mabomba kwa ajili ya ujenzi wa
bomba la gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es salaam, ambapo
amekumbushia madhumuni ya mradi huo kuwa ni kuongeza upatikanaji wa gesi asilia
ili kuweza kuongeza uzalishaji wa umeme na matumizi mengine, ambapo alitolea
mfano uzalishaji wa umeme kwa sasa aliosema zaidi ya nusu ya nishati hiyo
inazalishwa kutokana na gesi asilia huku akisisitiza matumizi ya gesi asilia
katika kufidia pengo la mahitaji ya umeme kufuatia mabadiliko ya tabia nchi.
Dk. Lu YouQing, Balozi wa China - Tanzania
|
Profesa Sospeter Muhongo - Waziri wa nishati na madini Tanzania. |
Katika kufanikisha
utekelezaji wa mradi huo kwa haraka, serikali imeamua kuupa kipaumbele kwa
kuuingiza katika mpango wake wa matokeo makubwa ya haraka sasa (Big Results
Now), ambapo ujenzi wake utachukua miezi kumi na minane na kukamilika mwaka
2014, ambapo utakuwa na uwezo wa kusafirisha futi za ujazo 784 kwa siku bila
mgandamizo na ukiwekwa mgandamizo utasafirisha futi za ujazo 1002 kwa siku.
0 comments:
Post a Comment