Esther Zelamula, Dar es salaam.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania
- JWTZ limethibitisha kwamba, askari saba wa Tanzania wakiwemo sita wa jeshi
hilo na mmoja wa Jeshi la Polisi Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi jana na kikundi cha waasi wa Sudan katika
eneo la Darfur nchini Sudan na askari wengine 14 wamejeruhiwa katika tukio
hilo.
Akithibitisha tuki hilo
katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania JWTZ Kanali KAPAMBALA MGAWE amesema wanajeshi hao ni
miongoni mwa walioko katika utekelezaji wa majukumu yao ya Umoja wa mataifa ya
Kulinda amani nchini Sudan, ambapo kikundi hicho cha askari wa Tanzania kikiwa
na afisa mmoja na maaskari 36 kilikuwa
katika msafara wa kusindikiza waangalizi wa Amani kutoka Khor Abeche kuelekea
Nyara eneo la Darfur, ambapo ghafla
kilishambuliwa na waasi hao umbali wa kilomita 20 kutoka makao makuu ya
kikosi hicho.
Kanali Kapambala Mgawe - Msemaji wa JWT Tanzania.
|
Kanali Mgawe amesema tayari
ujumbe maalum umeteuliwa kwenda Khartoum na Darfur kuzungumza na mamlaka
kuhusiana na tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kufanya mawasiliano kati ya JWTZ na
Umoja wa Mataifa kuhusu uwezekano wa kuongeza uwezo wa kujilinda na
mashambulizi inapobidi, pindi kikundi cha Tanzania kinapokabiliana na
mashambulizi ya aina hiyo.
Akielezea hatua
zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na JWTZ baada ya askari wa Tanzania
kushambuliwa katika tukio hilo na kutoa taarifa makao makuu ya Kikosi, Kanali
Kapambala Mgawe anasema;
Akijibu swali la mwandishi wa
habari aliyetaka kujua, ni namna gani ulinzi kwa askari wa Tanzania
uliimarishwa hasa suala zima na magari wanayotumia wawapo katika majukumu yao
ya kulinda amani, Kanali Mgawe alisema.
"Mazingira ya sasa yakule Dafur hapo katika hiyo chapter 7 ipo katika chapter 6 ambapo matumizi ya silaha yanakuwa relimited kwa sababu nikweli kama mnavyotambua ni muda mrefu tangu wamekwenda hawa askari na hapakuwahi kujitokeza hilo sasa Umoja wa mataifa unapo angalia hali hiyo baadae hua inabadilisha utaratibu na tunadhani tutashauriana nao ili waweze kubadilisha utaratibu ili tuwe katika Comfiguration nzuri zaidi yakuweza kupigana au kutumia nguvu ilikuweza kuokoa maisha ya watu" alisema Mgawe.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania
JWTZ lilikuwa na askari 875 wa kulinda amani Darfur nchini Sudan.
0 comments:
Post a Comment