Image
Image

IBRAHIM: ASEMA UCHAGUZI MKUU NCHINI ZIMBABWE UTAKUWA NI WAKIUSALAMA KUSINI MWA AFRIKA.







Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa, mafanikio ya uchaguzi mkuu ujao wa Zimbabwe, licha ya kuinufaisha nchi hiyo bali utakuwa na taathira ya kiusalama katika eneo lote la kusini mwa Afrika.

Ibrahim Ibrahim amesema kuwa, uchaguzi wa Zimbabwe uliopangwa kufanyika Julai 31 mwaka huu utapelekea kuboreka hali ya kiuchumi na kijami pamoja na kunyanyuliwa kiwango cha maisha ya wananchi wa Zimbabwe. 

Wananchi wa Zimbabwe wapatao milioni sita waliotimiza masharti ya kupiga kura, siku ya Jumatano ijayo wataelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kwa shabaha ya kumchagua rais pamoja na wabunge zaidi ya 200 na madiwani wapatao 2,000 nchini humo. 

Tume  ya Uchaguzi ya Zimbabwe imetangaza kuwa, mgombea wa  kinyang’anyiro cha urais  atakayepata asilimia 51 ya kura za wananchi atatangazwa mshindi, kinyume cha hivyo duru ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika mwezi Septemba.

Mchuano mkali wa nafasi ya rais unashuhudiwa kati ya rais wa sasa Robert Mugabe kutoka Zanu PF na Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu na ambaye pia ni kiongozi wa chama cha MDC.

  
Imeelezwa kuwa, hadi sasa karibu waangalizi 600 wa kigeni wako nchini Zimbabwe kwa shabaha ya kusimamia uchaguzi huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment