Image
Image

TIAKO YAPINGA MPANGO WA KUNDI LA KIMATAIFA LA KUTATUA MGOGORO MADAGASCAR





Chama cha 'Tiako I Madagasikara' kinachofungamana na Marc Ravalomanana rais wa zamani wa Madagascar kwa mara nyingine tena kimepinga mpango wa kundi la kimataifa la mawasiliano lililopewa jukumu la kuutatua mgogoro wa  Madagascar. 

Chama hicho kimesisitiza kuwa vitisho vya kundi hilo na jumuiya nyingine za kimataifa, havitaweza kubadilisha msimamo wa chama hicho. 

Mpango huo unawataka wagombea watatu wajiengue kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao wa rais nchini humo. 

Kundi la kimataifa la mawasiliano liliwataka Andry Rajoelina rais wa sasa wa serikali ya mpito ya Madagascar, Didier Ratsiraka rais wa zamani wa nchi hiyo pamoja na Lalao Ravalomanana mke wa Marc Ravalomanana rais wa zamani wa nchi hiyo wasishiriki kwenye uchaguzi ujao, kwani ushiriki wao  unakinzana na katiba ya nchi hiyo.  

Baada ya kufanyika mapinduzi nchini  Madagascar yapata miaka mitano iliyopita, na kuundwa serikali ya mpito, nchi hiyo imekuwa ikishuhudia migogoro ya kisiasa siku hadi siku.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment