Image
Image

JAMHURI YA KIISLAMU IRAN YATOA POLE KWA SERIKALI YA UHISPANIA KUFUATIA AJALI YA TRENI ILIYOTOKEA NCHINI HUMO.





Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Uhispania kutokana na ajali ya treni iliyotokea hivi karibuni nchini humo na kupelekea watu wasiopungua 80 kufariki dunia na wengine wasiopungua 140 kujeruhiwa 20 na hali zao zikielezwa kuwa  mahututi. 

Sayyid Abbas Araqchi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, ajali hiyo ya treni imeleta majonzi ulimwenguni kote, hivyo serikali pamoja na wananchi wa Iran wanaungana na wenzao wa Uhispania kwenye kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombelezo.

Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatano, pale treni hiyo ilipo kuwa inatembea mwendo wa kasi  katika kona na kusababisha mabehewa 13 kuondoka kwenye reli, na manne kupinduka kabisa. 

Taarifa zinasema kuwa, dereva wa treni hiyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ingawa alishatoa tahadhari ya kuanguka kwa treni hiyo, baada ya kushindwa kuidhibiti treni hiyo iliyokuwa kwenye  mwendo wa kasi. 

Treni hiyo ilikuwa ikitoka Madrid na kuelekea El Ferrol, na kupata ajali katika mji wa Santiago de Compestela, ulioko katika mkoa wa Galicia.

Hii inahesabiwa kuwa ajali mbaya zaidi ya treni kutokea nchini humo tokea mwaka 1972.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment