Image
Image

RAIS KIKWETE: HALIMASHAURI INGIZENI MPANGO WA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA ZA MWANZO KWENYE BAJETI ZENU




Rais Jakaya Kikwete,akiweka ngao na sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika kambi ya Jeshi la Wananchi ya kaboya,Bukoba,mkoani Kagera.


Rais Kikwete ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaingiza katika bajeti zao mpango wa ujenzi wa majengo ya Mahakama za Mwanzo ili kukabiliana na ukosefu na uchakavu wa majengo ya kuendeshea kesi.

 Alitoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba, uliofanyika jana na kuhudhuriwa na viongozi akiwamo Jaji Mkuu, Othuman Chande na Mawaziri.

Agizo hilo la Rais kikwete limekuja muda mfupi baada ya hotuba ya Jaji Mkuu kueleza kuwa Mahakama za Mwanzo 960 zilizopo nchini ni 664 ndizo zinazotumia majengo yanayomilikiwa na Mahakama huku 286 zikiendesha shughuli zake katika majengo ya taasisi nyingine za Serikali.

Hata hivyo alisema mahakama hizo baadhi zinatumia majengo ya Serikali za vijij,kata na majengo 10 yakiwa yanakodishwa toka kwa watu binafsi.

Akizungumzia Mahakama za Wilaya, Jaji Chande alisema 27 zinatumia majengo ya taasisi mbalimbali za Serikali na mahakama tatu ziko katika majengo ya kukodi huku Wilaya 32 nchini zikiwa hazina majengo ya mahakama za Wilaya kabisa.

Alimweleza Rais Kikwete kuwa lengo la Mahakama kuu ni kuwa na Mahakama Kuu katika mikoa yote chini na kwamba kwa sasa ni mikoa 13 tu ndiyo yenye Mahakama Kuu.

Aliitaja mikoa isiyokuwa na Mahakama Kuu kuwa ni Lindi, Shinyanga, Mara, Singida, Morogoro, Manyara, Pwani, Lindi, Geita, Simiyu, Njombe na Katavi.

Kutokana na maelezo hayo, Rais Kikwete alisema Serikali katika bajeti ya mwaka huu, imetenga fedha kwa ajili ya kumaliza mahakama saba likiwamo jengo la kanda ya Bukoba ambalo lilizinduliwa jana.

Alisema Serikali imedhamiria kwamba katika kipindi cha miaka miwili, suala la ukosefu wa Mahakama Kuu liwe historia hapa nchini angalau ili kuondoa kero kwa wananchi wanasafiri mikoa mingine kutafuta haki yao.

Wakati huo huo, Rais Kikwete aliongoza Watanzania nchini kuhudhuria maadhimisho ya mashujaa waliopigana vita vya ukombozi dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Nduli Idd Amini mwaka 1978/79, yaliyofanyika katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kaboya wilayani Muleba.

Rais Kikwete alitoa onyo kwa yeyote atakayejitia kiburi kwa kuchokoza serikali ya Tanzania na kusema kwamba nguvu zilizomwondoa Nduli Idd Amini ndizo hizo zitakazotumika kumsughulikia.

Aliwataka Watanzania kulala usingizi bila kuwa na hofu juu ya wachokozi.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwasalimia wananchi waliokuwa katika viwanja hivyo, aliwatoa hofu wananchi akieleza kwamba jeshi liko imara wakati wote na muda wote.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment