Image
Image

IBRAHIM: TUTAWATOA KINGUVU WAFUASI WA MURSI.


Waandamanaji wanaomuunga mkono rais  Muhammad Mursi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya mpito ya Misri, Mohammad Ibrahim amesema kuwa, maafisa wa usalama wanajiandaa kuwatawanya waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa, Muhammad Mursi. 

Ibrahim amesema vyombo vya usalama vitafanya hivyo kwa mujibu wa sheria na kwamba mikakati imewekwa ili kuhakikisha hakuna umwagikaji wa damu utakaotokea kwenye oparesheni hiyo. 

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amesema wananchi walijitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kwenye medani ya Tahrir wameipa serikali idhini na baraka ya kuwaondosha kwa nguvu wafuasi wa Mursi. 

Hii ni katika hali ambayo, wafuasi wa kiongozi huyo aliyepinduliwa wameapa kuendelea kukaa nje ya msikiti wa Rabaa Al-Adawiya katika mji wa Nasr ulioko viungani mwa Cairo hadi pale Dkt. Mursi atakaporejeshwa madarakani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment