Image
Image

CHIKAWE: BILA SHERIA MPYA YA UCHAGUZI TANZANIA ITAYUMBA.


Mathias Chikawe
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Mathias Chikawe, amesema kama Watanzania watakubali muundo wa serikali tatu uliopendekezwa katika Rasimu ya Katiba Mpya, kutahitajika mabadiliko makubwa ya kisheria na kitaasisi ili kuwa na sheria nzuri zitakazodhamini uchaguzi huru na wa haki  mwaka 2015. 

Kiongozi huyo amekanusha tuhuma alizoelekezewa na vyombo vya habari kwamba anao ushahidi unaoonyesha kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga kuchelewesha uchaguzi ujao. 

Amesema muundo wa serikali tatu ukikubaliwa utahitaji muda wa maandalizi ingawa hiyo haina maana kwamba uchaguzi usongezwe mbele. 

Waziri Chikawe ametahadharisha juu ya muundo wa serikali 3 na kuwataka Watanzania watathmini kwa makini matokeo yake, changamoto, gharama na natija ya muundo huo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.  
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment