Image
Image

JESHI LA POLISI LAKANUSHA KUVAMIWA NA KUPIGWA MAWE GARI LILILOKUWA LIMEBEBA MABOMBA YA GESI MTWARA.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara Linus Simzumwa amekanusha taarifa za kuvamiwa na kupigwa mawe na watu wasiojulikana gari lililokuwa limebeba mabomba ya mradi wa ujenzi wa kusafirishia gesi asilia kutoka mtwara kwenda Dar .
Linus Simzumwa Kamanda wa polisi Mtwara.

Likiwa limebeba mabomba sita kuyapeleka kituo cha Kilanjelanje mkoani Mtwara ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa mradi huo wa bomba, kioo cha mbele cha roli la kampuni kutoka China ya CPDC inayojenga bomba hilo kilivunjwa kwa jiwe.

Akitolea ufafanuzi tukio hilo, Kamanda Simzumwa amesema kuvunjika kioo cha mbele cha lori hilo kulitokana na mwendo kasi wa kupishana kwa magari na kwamba jeshi hilo linaendelea na upelelezi.
Kwa upande wake dereva wa roli hilo Said Mohammed pamoja na kuthibitisha kuvunjwa kwa kioo cha gari hilo amesema hafahamu chanzo cha kutokea kwa jiwe hilo.

Shughuli za ujenzi wa bomba la gesi zimeanza rasmi kwa kampuni ya china kueneza mabomba hayo kwenya kambi zilizotengwa.
 Aidha amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuligeuza soko hilo kuwa la kimataifa zaidi bila kuchagua mfanyabiashara mdogo au mkubwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment