Image
Image

NANDO ATIMULIWA NDANI YA JUMBA LA BBA BILA HURUMA.


                                                                       Nando 


Mshiriki kutoka nchini Tanzania Nando ametimuliwa katika jumba la Big Brother baada ya kudumu kwa wiki tisa sasa.
Sheria za mwaka huu katika jumba hilo la Big Brother zimekuwa za tofauti kwani mshiriki haruhusiwi kufanya kosa kubwa ambalo litampelekea kupata "strike" Onyo.
Nando alikutwa na kisu alipoingia katika studio z channel O, na licha ya kukutwa na kisu nando aligombana na mshiriki mwenzake Elikem ugomvi ambao Nando ndo aliyekuwa mwanzilishi.

Hata hivyo inaelezwa kuwa  Nando amekutwa amelala na mkasi kitandani jambo liloshangaza wengi na kutokana na kuwa na sharia kali bac ilibidi atimuliwe kwani visanga vilizidi ndani ya jumba hilo la BBA.

Pia nando alionekana ni kijana ambaye alikuwa hajiamini na pengine kila aliye karibu naye alionekana kuwa adui yake kwa namna moja ama nyingine. "A troubled young Man" kama alivyomwelezea Big Brother mwenyewe.
Kwa mujibu wa sheria hizo mpya, mshiriki atakayepewa onyo mara tatu atapewa adhabu ya kutimuliwa katika mashindano hayo ya Big Brother the Chase.

Aidha nando amefanya makosa mara tatu hivyo ametimuliwa rasmi.

Pamoja na hivyo, Big brother imetoa onyo kwa yeyote atakayefanya fujo atatimuliwa mara moja ndani ya BBA bila huruma.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment